Home  News & Events
News & Events
PSPF ANNUAL GENERAL MEETING
Published On: 26th Feb 2014

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinti, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto), akimkaribisha mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimatifa, John Haule alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014

 

 

 

 

 

 

 

 

Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC, John Haule 

 

 

Wadau wakisikiliza Mkutano unavyoendelea

SALAMU ZA PONGEZI
Published On: 21st Jan 2014

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SALAMU ZA PONGEZI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.


Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.

Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.
PSPF - Tulizo la Wastaafu

Mkurugenzi Mkuu

Mfuko wa Pensheni - PSPF

PSPF PAMOJA NAWE
Published On: 15th Jan 2014

PSPF PAMOJA NAWE Fungua kuona zaidi

Ndugu mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, sasa unaweza kupata huduma mbalimbali kutoka kwenye Mfuko kwa kutumia simu yako ya mkononi kupitia huduma ya PSPF Kiganjani.

Huduma unazoweza kupata ni kama zifuatazo:

1.     Kuhakiki Usajili - Kuangalia taarifa yako ya usajili kwenye Mfuko

2.     Historia ya Michango - Kuangalia taarifa za michango yako ya kila mwezi katika Mfuko.

3.     Historia ya Pensheni - Kuangalia taarifa za malipo yako ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu na wategemezi.

4.     Kufuatilia Mafao – kuangalia hatua ya ukokotoaji wa mafao uliyoomba

5.     Sajili - Kujisajili katika Mfuko

 

Kwa kuanzia, huduma hii itapatikana kwa wale waliojiunga katika Mitandao ya Vodacom na Airtel.

Jinsi ya kutumia huduma hii ya PSPF KIGANJANI:

a.     Kwa kutumia simu yako ya mkononi tuma Meseji ‘PSPF’ kwenda namba 15357.

b.     Utapokea orodha ya huduma zifuatazo:

 

1. Hakiki Usajili

2. Historia Michango

3. Historia Pensheni

4. Fuatilia Mafao

5. Sajili

Jibu 1,2,3,4,5 ikifuatiwa na namba ya uanachama. au 5 ikifuatiwa na jina lako na makazi

d.     Jibu kwa meseji kwenda namba 15357 kulingana na huduma unayotaka.

 

Mfano kuhakikisha usajili       bonyeza  1   4000123567

Mfano kusajili na PSPF           bonyeza  5  

Hamisi Juma,                    Temeke, Dar es Salaam


PSPF Member kutoka USA na Canada
Published On: 31st Dec 2013

Eliserena Kimolo awapatia PSPF members kutoka Canada Mr. Stephan Kakete and Mrs. Milca Kakete

 

 


Chini: Eliserena Kimolo awandikisha Pastor Melchizedek Maturu pamoja na wengine kuwa member wa PSPF

Thank you ! We have received your message.
Feedback Form
Full Name:
Email Address:
Comments:
 
 
 
Member AccessNews & Events
26th February 2014
 PSPF ANNUAL GENERAL MEETING
  
21st January 2014
 SALAMU ZA PONGEZI
  
15th January 2014
 PSPF PAMOJA NAWE
  
31st December 2013
 PSPF Member kutoka USA na Canada
  
6th December 2013
 MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA
  
29th November 2013
  USA - DIASPORA PRESENTATION
  
 
Copyright © 2003 - 2014 Public Service Pension Fund. All Rights Reserved.  Privacy Policy   |  Disclaimer  |  Contact Us  |  Feedback  |  Sign Up