Home  News & Events
News & Events
HOUSES FOR PSPF MEMBERS
Published On: 29th May 2013

MAUZO YA NYUMBA ZA PSPF

Mfuko unapenda kuwataarifu wananchi wote kwamba inauza nyumba zilizojengwa na Mfuko katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba) na Shinyanga (Ibadakuli).

Bei ya nyumba ni kati ya Tsh 59,000,000.00 hadi Tsh 80,000,000.00 (Bila ya VAT) kulingana na ukubwa wa nyumba na Mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu tano (TShs. 5,000/=) kwenye ofisi za Mfuko zilizopo mikoa yote nchini.

Waombaji wanaohitaji kuona na kukagua nyumba wawasiliane na Mfuko kupitia namba 2120912/52 au 2127376.

“PSPF - Tulizo la Wastaafu”

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu,

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),

Golden Jubilee Towers,

Front Tower – Ghorofa ya 6-13,

Mtaa wa Ohio/Kibo,

S. L. P. 4843,

DAR ES SALAAM.

Barua Pepe: pspf@pspf-tz.org           Tovuti: www.pspf-tz.org  

Mkutano Mkuu wa Wadau wa PSPF
Published On: 21st Mar 2013

 

Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wadau wa PSPF, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiweka sahihi katika kitabu cha wageni.  Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF ndugu George Yambesi. 

 


 
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadhan Dau akibadilishana Mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa PPF ndugu William Erio wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wadau wa PSPF.  
   


 
Washiriki wa mkutano wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau  
   


 
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Wadau wa PSPF wakijisajili kabla ya kuanza kwa mkutano.  

 

 

 

 

Stakeholders visited PSPF Low Cost Houses
Published On: 25th Feb 2013
http://3.bp.blogspot.com/-BuhZBrlCQks/USdZbx94VmI/AAAAAAAAEn8/r1CYZvtYoS0/s1600/3.jpg
 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Mujibu wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Mfuko umejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzi wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo la Thamani.

   http://3.bp.blogspot.com/-pzUYcdOrVAI/USdZbyIrceI/AAAAAAAAEoA/uLp7FMvsDzQ/s1600/2.jpg
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

 

http://2.bp.blogspot.com/-qzOpFaE0g9c/USdZhsvWfEI/AAAAAAAAEoU/L1WklrIyFIM/s1600/5.jpg
 Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.http://1.bp.blogspot.com/-BvyXWntdwlM/USdZhx8OsKI/AAAAAAAAEoY/adLC4WN0o2g/s1600/6.jpg Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491

Supplementary Scheme
Published On: 22nd Feb 2013

Mabadiliko katika sekta ya hifadhi ya jamii yamepelekea kuwepo na mabadiliko ya sheria ya Mfuko. Sheria ya Mfuko inaruhusu kusajili wanachama katika sekta zote za umma na binafsi. Mfuko sasa utakuwa na mpango wa uchangiaji wa lazima (PSPF Mandatory Scheme) na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF Supplementary Scheme)

PSPF Supplimentary Scheme, Mwanachama atapaswa kuchangia si chini ya Tshs 10,000 kwa mwezi. Michango inaweza kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi au awamu. Mwanachama atawekewa gawio la akiba yake kwa kila mwaka mara moja. Uanachama ni kwa watanzania wote na wasio watanzania wanaofanya kazi nchini na hata waliopo nje ya nchi. Wanachama waliokwisha kujiunga na Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii ikiwemo PSPF wanaweza kujiunga na mpango huu. Jiunge sasa ufaidike

Thank you ! We have received your message.
Feedback Form
Full Name:
Email Address:
Comments:
 
 
 
Member AccessNews & Events
26th February 2014
 PSPF ANNUAL GENERAL MEETING
  
21st January 2014
 SALAMU ZA PONGEZI
  
15th January 2014
 PSPF PAMOJA NAWE
  
31st December 2013
 PSPF Member kutoka USA na Canada
  
6th December 2013
 MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA
  
29th November 2013
  USA - DIASPORA PRESENTATION
  
 
Copyright © 2003 - 2014 Public Service Pension Fund. All Rights Reserved.  Privacy Policy   |  Disclaimer  |  Contact Us  |  Feedback  |  Sign Up