Viunganishi    

KUFAHAMU HIFADHI YA JAMII

SW. HIFADHI YA JAMII NI NINI?

JIBU. Kwa mujibu wa maelezo ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) Hifadhi ya Jamii ni hatua ya Kinga ambayo jamii inatoa kwa wanachama wake, kupitia mfululizo wa hatua za umma dhidi ya matatizo ya kiuchumi na kijamii ambayo yanaweza kusababishwa na kusimamishwa kazi au kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mapato kunakotokana na ugonjwa, uzazi, kuumia kazini, ukosefu wa ajira, ulemavu, uzee, kifo, utoaji wa msaada wa huduma za afya kwa familia zenye watoto.

Mafao ya kulinda kipato yanayotolewa chini ya programu ya hifadhi ya jamii kwa asili ni fedha.

SW. NINI UTARATIBU MPANGO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA NI NINI?

JIBU.Ni utaratibu wa uchangiaji wa pensheni ambao wanachama huchangia kwa kila mwezi na kupata mafao yao pale watakapostahili.

SW. MPANGO HUU UNAGHARIMIWAJE?

JIBU: Mpango huu unagharimiwa kwa michango kutoka kwa waajiri, wafanyakazi na mapato ya vitegauchumi vinavyomilikiwa na mfuko.

SW: JE, NI KIWANGO GANI CHA MICHANGO KINATOLEWA?

JIBU: Kila mfanyakazi anatakiwa kutoa mchango wa 5% ya mshahara wake wa kila mwezi, wakati ambapo kila mwajiri anatakiwa kutoa mchango wa 15% ya mshahara wa mfanyakazi wa kila mwezi kwa kuzingatia mfanyakazi huyo.

SW: JE, MICHANGO INALIPWAJE?

JIBU: Michango ya wafanyakazi inatakiwa kulipwa katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya mwisho wa mwezi, katika siku ya mwisho ya kipindi cha kuchangia.

SW: NI NAMNA GANI MICHANGO HIYO HULIPWA KATIKA MFUKO?

JIBU: Michango hiyo italipwa kwa hundi, fedha taslimu katika ofisi za PSPF, uhamishaji wa telegrafiki na njia za kielektroni kwa wataalamu wa Benki wa PSPF na NMB.

SW: JE, MWANACHAMA ANAWEZA KUTOA SEHEMU YA MCHANGO WAKE?

JIBU: Hapana, mwanachama hawezi kutoa sehemu ya michango yake kwa sababu siyo utaratibu wa kuweka akiba.

Michango inatakiwa kufanywa kwa kipindi cha muda fulani kilichowekwa ili kuwezesha mpango kulipa mafao yaliyowekwa dhamana chini ya utaratibu.

Inatambulika, kama sehemu ya malimbikizo ya michango imetolewa fedha za mpango zitapunguzwa na haitawezekana kutoa mafao yaliyoahidiwa.

KAZI ZA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA

SW: MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF) HUFANYA NINI?

JIBU: Mfuko hufanya kazi maalumu zifuatazo:

  • Kusajili wanachama wote;
  • Kusajili waajiri wote;
  • Kukusanya michango ya wanachama na kuziweka pamoja data zinazohusiana na michango;
  • Kusimamia na kuwekeza fedha
  • Kutunza na kurekebisha kumbukumbu zinazohusu wanachama.
  • Kulipa mafao pale yanapotakiwa.

WANACHAMA WA MFUKO

SW: MWANACHAMA WA MFUKO NI NANI?

JIBU: Wafanyakazi wote wa Serikali Kuu na Wakala Tendaji walioajiriwa kwa masharti ya pensheni wanaweza kuwa wanachama wa mfuko ikiwa ni pamoja na wale waliohamishiwa kwa muda katika taasisi nyingine.

SW: JE, KAMA MWANACHAMA NITAJISAJILI WAPI?

JIBU: Wewe kama mwanachama unaweza kujisajili katika Ofisi za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma zilizoko katika Jengo la Sukari (Sukari House) ambalo lipo kona ya Mtaa wa Ohio na Sokoine, Dar es Salaam au kwa kufanya mipango kati ya mwajiri na PSPF ambapo zoezi la usajili linaweza kufanyika katika ofisi za waajiri wakiwepo maofisa wa PSPF.JIBU: Wewe kama mwanachama unaweza kujisajili katika Ofisi za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma zilizoko katika Jengo la Sukari (Sukari House) ambalo lipo kona ya Mtaa wa Ohio na Sokoine, Dar es Salaam au kwa kufanya mipango kati ya mwajiri na PSPF ambapo zoezi la usajili linaweza kufanyika katika ofisi za waajiri wakiwepo maofisa wa PSPF.

Kama wewe ni mfanyakazi wa Wakala Tendaji utahitaji barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri.

SW: JE, UNATAKIWA KUJISAJILI TENA IKIWA UMEBADILI KAZI AU MWAJIRI?

JIBU: Hapana, unatakiwa kujisajili mara moja tu. Kama umesajiliwa na una namba ya hundi ya mshahara au yenye namba ya PSPF, na kama umebadili kazi, tafadhali mfahamishe mwajiri wako mpya kuhusu uanachama wako katika mpango na mruhusu aiandike namba ya hundi ya mshahara wako au namba ya kitambulisho cha PSPF katika miamala na PSPF.

SW: JE, MTU MWINGINE ANAWEZA KUTUMIA NAMBA YA CHEKI YAKO YA MSHAHARA?

JIBU: Hapana, Namba ya cheki ya mshahara ni ya mwanachama pekee na haiwezi kutumika na mtu mwingine isipokuwa kwa mtu ambaye namba hiyo imetolewa. Namba ya cheki ya mshahara lazima inakiliwe katika miamala yote inayohusisha mwanachama na PSPF.

Hakikisha kwamba namba yako sahihi inanakiliwa katika silipu ya malipo.

Kama mwajiri wako anakata michango yako ya pensheni ya kila mwezi lakini huna namba ya cheki ya mshahara au namba ya kitambulisho cha PSPF tafadhali wasiliana na ofisi za PSPF kwa ushauri.


KUHUSU KUMBUKUMBU BINAFSI

SW: JE, UNATAKIWA KUIFAHAMISHA PSPF KAMA UMEBADILI JINA?

JIBU: Ndiyo, mwanachama yeyote anayebadili jina lake anatakiwa kuwasiliana na ofisi za PSPF ili mabadiliko hayo yaingizwe katika kumbukumbu binafsi katika PSPF.

SW: JE, UNATAKIWA KUIFAHAMISHA PSPF PALE UNAPOBADILI ANWANI YAKO?

JIBU: Ndiyo, kama umebadili anwani yako, tafadhali zifahamishe ofisi za PSPF kwa mabadiliko kuingizwa katika kumbukumbu binafsi.

SW: JE, UNAWEZA KUBADILI TAREHE YAKO YA KUZALIWA NA PSPF?

JIBU: Hapana, tarehe ya kuzaliwa haiwezi kubadilishwa.

SW: JE, NI MARA NGAPI MWANACHAMA ANABADILI WANUFAIKA?

JIBU: Mara nyingi kadri inayowezekana.

MAFAO

SW: KUNA MAFAO GANI KATIKA MPANGO WA PENSHENI WA PSPF?

JIBU: Mafao ni haya yafuatayo:

SW: NI KITU GANI HUAMUA KIASI CHA MAFAO?

JIBU: Mpango unahusiana na mshahara, na kiasi cha mafao kinaamuliwa na muda wa mchango.


HITIMISHO

Kwa maswali zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi za PSPF, ghorofa ya 4, Jengo la Sukari, Kona ya Mtaa wa Ohio na Sokoine S.L.P. 4843, Dar es Salaam au kwa simu 022 2120912.

 

 

  © 2003 PSPF All rights reserved.