Viunganishi    
 

Kifungu cha 53 (b) cha sheria Na. 2 ya Mafao ya Watumishi wa Umma wastaafu ya mwaka 1999 inaeleza moja kati ya kazi kuu za PSPF ambayo ni "kuwekeza fedha za Mfuko zilizopo." Ili kufanya kazi hii Mfuko umeanzisha sera ya usimamizi wa kitegauchumi ambayo ni pana kama mwongozo wa kuendesha vitegauchumi vyake mbalimbali.

Sera inalenga katika kupata na kutunza kiasi halisi cha faida katika orodha ya fedha zilizowekwa kwa faida pamoja na kuendeleza orodha ya vitegauchumi mbalimbali ambavyo vina uwezo wa kuongoza majukumu ya Mfuko ya muda mfupi na mrefu katika misingi endelevu.

Malengo ya Sera

  • Kuongeza faida thabiti katika Mfuko na kuwa na uangalifu mkubwa katika madhara;
  • Kuhakikisha kwamba kuna raslimali za kutosha ili kufikia dhima ya pensheni ya mfuko;
  • Kuhakikisha ufaaji wa mali za mfuko kulingana na mahitaji ya mfuko;
  • Sera inalenga katika kupata faida kubwa katika vitegauchumi ikiwa na
    kiasi kidogo cha madhara.
Usalama: PSPF itawekeza mahali ambapo pana usalama wa Mtaji wa Mfuko.
Mazao: Faida katika vitegauchumi lazima iwe inakubalika.
Uwezo wa: PSPF itahakikisha kwamba raslimali za kutosha zinawekwa
Kupata Fedha katika vitegauchumi vya muda mfupi ili kuwezesha Mfuko
kufikia malengo yake.
Matumizi ya Kiuchumi na kijamii Ni katika maslahi ya Mfuko kuhakikisha kwamba kiasi
fulani cha fedha kinawekezwa kwa namna ambayo
kitachangia katika kuboresha hali ya Elimu na Afya au hali ya maisha ya
Wanachama.

Upanuzi:

Kuhakikisha kwamba orodha ya fedha zilizowekezwa kwa faida zinaelekezwa katika hali ya kubadilisha mazingira.

Orodha ya vitegauchumi

Orodha ya vitegauchumi vya Mfuko imepangwa katika makundi mawili makubwa; vitegauchumi vya mapato ya kudumu na vitegauchumi vya mapato ya yasiyo ya kudumu. Kwa kuzingatia makundi haya, mfuko umelenga katika kutumia aina za fedha na viwango vifuatavyo


Aina za fedha na viwango vilivyopendekezwa kwa mwaka 2002/3 - 2004/5

Mali Kima chini* Lengo la kimkakati Kima juu*
A: PATO LA KUDUMU      
Hawala ya serikali 15 25 35
Dhamana za serikali 15 20 30
Amana za muda maalumu 10 15 25
Mikopo ya ushirika 3 5 10
Jumla ndogo   65  
B: PATO LISILO LA KUDUMU      
Hisa: -      

Zilizoorodheshwa

5 10 20
Zisizoorodheshwa 2 8 10
Mali halisi 5 10 20
Dhamana za shirika   2 25
Miundombinu*   5 10
Jumla ndogo   35  
       
Jumla kuu   100  

 

* Jumla ya kimachini na kimajuu hakilingani na asilimia 100 kwa sababu mabadiliko kutoka katika mgawanyo wa malengo lazima yafidiwe na kinyume cha mabadiliko.

** Haya ni maeneo mapya ya vitegauchumi yaliyopendekezwa.


 

 

 

  © 2003 PSPF All rights reserved.  
Investment Policy Current Investment