Viunganishi    

Menejimenti ya PSPF

Bodi ya Wadhamini inawajibika kwa ajili ya menejimenti na usimamizi wa Mfuko kufuatana na masharti ya sheria ya mafao ya Watumishi wa umma wastaafu Na. 2 ya mwaka 1999. Chini ya Bodi kuna timu ya Menejimenti ambayo inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu, ambaye anawajibika katika usimamizi wa kila siku wa Mfuko.

Bodi ya Wadhamini

Mchanganyiko wa wajumbe wa Bodi ni sheria iliyotolewa chini ya sheria iliyoanzisha Mfuko.

Wajumbe hawa ni pamoja na:

  • Katibu Mkuu wa hazina ambaye ni Mwenyekiti;
  • Katibu Mkuu wa Utumishi;
  • Mwanasheria Mkuu;
  • Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania;
  • Katibu Mkuu wa TUGHE;
  • Msajili wa Hazina;
  • Wajumbe wengine watatu walioteuliwa na Waziri wa Fedha, wawili wakiwa
  • wawakilishi wa TUGHE ambao mmoja wao anatakiwa kuwa mwanamke, na mwakilishi mmoja kutoka Utumishi.


Menejimenti

Uendeshaji wa kila siku wa mfuko ni jukumu la Mkurugenzi Mkuu ambaye anatoa ripoti katika Bodi ya Wadhamini. Mkurugenzi Mkuu husaidiwa na Wakuu wa Kurugenzi na Vitengo.

Kuna Kurugenzi nne na vitengo viwili kama ifuatavyo:

  • Kurugenzi ya uendeshaji
  • Kurugenzi ya Mipango na Vitegauchumi
  • Kurugenzi ya Mfumo wa Taarifa
  • Kurugenzi ya Fedha na Utawala
  • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Kitango cha huduma za Kisheria.


Jedwali la Muundo

Muundo wa Mfuko umeonyeshwa hapa chini:


  © 2003 PSPF All rights reserved.