Viunganishi    

UTANGULIZI

Ni utaratibu wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa na sheria ya mafao ya watumishi wa Umma wastaafu Na. 2 ya mwaka 1999 ili kuibadili ile sheria ya Pensheni, Sura ya 371 ya mwaka 1954.

WAHUSIKA

Wanachama wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma ni Wafanyakazi wa serikali walioajiriwa Tanzania na wafanyakazi walioajiriwa na Wakala Tendaji zilizoanzishwa chini ya sheria ya Bunge.

DIRA

Kuwa taasisi imara ya Hifadhi ya Jamii nchini katika raslimali na mtoaji wa hifadhi ya jamii anayefaa katika kutoa huduma bora kwa wanachama.

DHAMIRA

Kutoa huduma za hifadhi ya jamii zenye ushindani kwa wanachama wetu katika hali ya kufaa na ufanisi kwa kutumia watumishi waliojitoa kwa dhati na Teknolojia ya inayofaa.

MAADILI

· Kutoa huduma yenye ubora wa hali ya juu, haraka, kwa ufanisi na heshima;
· Kuwa raia wenye ushirikiano wanaofanya kazi kwa maslahi ya wanachama wetu;
· Kuwa watumishi wenye wajibu katika fedha ambazo tumewakabidhi;
· Kukuza uwajibikaji na ubunifu katika kushirikisha mahitaji ya wanachama wetu.

LENGO

Lengo la Mfuko ni kutoa kwa ajili ya michango na malipo ya pensheni, kiinua mgongo na mafao mengine kulingana na huduma kwa wafanyakazi wote wa serikali wanaostahili Pensheni na wale wote walioajiriwa na Wakala Tendaji.

UTARATIBU

Mfuko wa pensheni kwa watumishi wa Umma ni utaratibu wa mafao bayana ya hifadhi ya jamii unaofanya kazi kwa mujibu wa kanuni za Bima ya Jamii. Wanachama wa Mfuko wanachangia kwa vipindi na kupata mafao yao pale watakapostahili.

UGHARIMIAJI

Vyanzo vya mapato ni:-
· Michango ya wafanyakazi ya 5% ya mshahara msingi
· Michango ya waajiri ya 15% ya mshahara msingi wa mfanyakazi
· Fedha zinazotokana na vitegauchumi vya Mfuko
· Fungu la fedha linaloweza kuidhinishwa na Bunge kwa madhumuni ya Mfuko
· Tathmini ya Mapato na Mtaji vinavyopatikana kutokana na umilikaji wa mali za Mfuko.

MAFAO YANAYOTOLEWA CHINI YA UTARATIBU

  • Mafao ya Uzeeni
  • Mafao ya Ugonjwa
  • Mafao ya Kifo na Pensheni kwa wanaobaki
  • Mafao ya Msaada wa mazishi
  • Mafao ya Kujitoa.

MAFAO

Lengo la Mfuko wa pensheni ni kutoa kipato badili kwa watu ambao wamepoteza moja kwa moja kipato chao.

MAFAO YA UZEENI

Ni mafao yanayolipwa kwa mwanachama aliyefikisha umri miaka 55 au 60 kwa hiari au kwa lazima.

MAFAO YA UGONJWA

Dhana ya ugonjwa inajikita katika kupoteza uwezo wa kutafuta kipato kutokana na kutokuwa na uwezo. Tathmini ya ugonjwa itafanywa na Bodi ya kuchunguza Afya iliyoanzishwa.

MAFAO YA WANAOBAKI

Mafao yanalipwa kwa wategemezi wa marehemu aliyekuwa mwanachama. Wategemezi hao ni pamoja na mke/mume, watoto na wazazi wa ofisa aliyefariki. Mafao kwa wanaobaki hulipwa bila kuathiri sheria za mirathi zilizopo.

MAFAO YA KIFO

Pale mwanachama anapokufa akiwa katika utumishi Bodi itampa yule mwakilishi wa kisheria kiasi chochote cha fedha kisichozidi ama mshahara wake wa mwaka unaostahili pensheni au kupunguza katika pensheni ya kiinua mgongo, kama ipo chochote kitakachokuwa kikubwa.

MSAADA WA MAZISHI

Msaada wa mazishi utatolewa kwa wanafamilia wa mwanachama aliyefariki kama rambirambi.

MAFAO YA KUJITOA HUZINGATIA:

  • NDOA
    Hulipwa kwa mwanachama mwanamke anayeolewa kufuatia kuacha kazi yenye kipato kizuri
  • UZAZI
    Hulipwa kwa mwanachama mwanamke aliyezaa mtoto na ameacha kabisa kazi yenye kipato kizuri
  • UHAMAJI AU KUKOSA KAZI
    Hulipwa kwa mwanachama anayehama au aliyehama kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

  © 2003 PSPF All rights reserved.